Proverbs 24:14-20

14 aUjue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako,
kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo,
nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.

15 bUsivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia
makao ya mwenye haki,
wala usiyavamie makazi yake,
16 cKwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena,
lakini waovu huangushwa chini na maafa.

17 dUsitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo;
wakati ajikwaapo,
usiruhusu moyo wako ushangilie.
18 e Bwana asije akaona na kuchukia
akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.

19 fUsikasirike kwa sababu ya watu wabaya
wala usiwaonee wivu waovu,
20 gkwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo,
nayo taa ya waovu itazimwa.
Copyright information for SwhNEN